MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA KOROGWE ANATANGAZA NAFASI ZA KAZI KWA MAFUNDI UJENZI WENYE UZOEFU WA KUTOSHA KUJENGA MAJENGO YA SERIKALI.
SIFA ZA MWOMBAJI:
1. AWE RAIA WA TANZANIA
2. AWE NA UMRI WA MIAKA KUMI NA NANE (18) NA KUENDELEA.
3. AWE HAJAWAHI KUTUHUMIWA NA KUFUNGWA.
4. AWE NA UZOEFU NA UJENZI WA MAJENGO YA SERIKALI.
5. AWE NA VIFAA VYA KAWAIDA VYA FUNDI UASHI.
6. AWE ANAJUA KUSOMA NA KUANDIKA.
7. AWE NA UWEZO WA KUSOMA RAMANI NA KUITAFSIRI.
8. AWE HAJAWAHI KUSHINDWA KUFANYA KAZI ALIZOPEWA KWA KUTOMALIZA KWA WAKATI.
9. MAFUNDI WENYEJI WATAPEWA KIPAUMBELE.
BARUA YA MAOMBI ITUMWE KWA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA KWA ANWANI IFUATAYO:
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
S.L.P 584
KOROGWE
MWISHO WA KUPOKEA BARUA YA MAOMBI NI JUMATANO TAREHE 06/02/2019 SAA 4:00 ASUBUHI. BAADA YA HAPO HAKUNA BARUA YOYOTE ITAKAYOPOKELEWA.
Limetolewa na:
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
Korogwe.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa