KAIMU mkuu wa wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe aliyesimama (kushoto) akizungumza na wananchi wa vijiji vya Lusanga na Mnyuzi mkutano ambao ulifanyika viwanja vya Mahakama Mnyuzi.
Wananchi walipata fursa kuwasilisha kero zao na walifunguka kwa kina kuhusu Sekondari yao licha ya ujenzi kukamilika Majengo kutokutumika.
Choo cha shule ya msingi Mnyuzi ujenzi wake kuchukua muda mrefu bila kukamilika licha ya wananchi kuchangishwa fedha na nguvu kazi.
Kero ya ukosefu nishati umeme Lusanga, Zahanati kukosa baadhi ya vipimo na uhaba wa watumishi nk.
Yote hayo yalipata majibu na wananchi waliridhia zaidi ya yote uongozi wa Zahanati umetakiwa kwenda Korogwe kupatiwa fedha ili baadhi ya vifaa kupatikana kuondoa changamoto.
Suala la mashamba ya Misufi lilitolewa ufafanuzi na wananchi kuelewa kwa kina huku milango ya ofisi ya DC na Mkurugenzi ikiendelea kuwa wazi kutatua changamoto za wananchi.
Wananchi wa Mnyuzi na Lusanga bado wanapewa kipaumbele kupata ardhi kwenye shamba hilo ili mradi tu wazingatie sheria stahiki pasipo kujihusisha na vitendo vyenye malengo ya kukwamisha mradi huo wa kisasa.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Dk George Nyaronga ameasa tabia ya baadhi ya watu kuvamia eneo hilo akisisitiza taratibu za sheria kufuatwa na kama kuna mtu ana hati ya kumiliki eneo hilo kufika ofisi za serikali ili haki iweze kutendeka.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa