Taasisi hiyo imesema hayo wakati wa kikao kupitia idara ya maendeleo ya jamii ambapo imewasilisha mpango kazi wa shughuli ambazo zinatekelezwa kwenye jamii.
Halfa hiyo ilihudhuriwa na Afisa Tarafa wa Mombo Ndg. Alex Mhando akimuwakilisha Mkuu wa wilaya korogwe ambapo aliipongeza taasisi hiyo kwa shughuli ambazo inatekeleza kwa jamii vilevile aliwasisitiza wataalam wa halmashauri kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuweza kufikia lengo la kuleta maendeleo kwa jamii.
Sambamba na hilo Ndugu.Alex alihimiza taasisi hiyo na wataalam wakati wa kutembelea vijana hao kusisitiza suala zima la uzalendo hasa katika kipind hichi ambacho taifa limepita katika kipindi cha uvunjifu wa Amani.

Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa