Mradi wa shule bora kuleta mapinduzi katika somo la hisabati na kiingera.Mapinduzi haya yanatarajiwa kufanyika mara baada ya kukamilika kwa mafunzo ya walimu wa shule za Msingi kujifunza Mbinu mbadala za kuinua ufaulu wa masomo hayo ambayo yamekuwa na ufaulu duni.Afisa Elimu awali na Msingi Mwl.Elias Mavoa amesema mafunzo haya yatakwenda kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu kwani kupitia mbinu hizo za kushusha maaarifa(cascade) ambapo walimu waliopatiwa mbinu hizo watakwenda kufundisha maarifa hayo kwa walimu wengine waliko Shuleni.
Mwalimu Aproni Chapuga wa shule ya Msingi Manka ni moja kati ya wanufaika wa Mpango huo.Kupitia shule Bora anaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kupatiwa mafunzo hayo kuwajengea uwezo kwenda kutekeleza Majukumu yao ipasavyo na kuinua ufaulu wa Wanafunzi katika masoma ya kiingereza na Hisabati

Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa