MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe Charles Mweta amewataka Wajumbe wa baraza la madiwani kushiriki misalagambo kwa vitendo hatua ambayo itahamaisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo yao.
Mweta alitoa rai hiyo alipozungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani akisema,madiwani watakaposhiriki misalagambo kwa vitendo wataamsha ari ya wananchi kushiriki utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo yao.
Aliwataka madiwani hao kuhakikisha kwamba wanashiriki misalagambo hiyo itakayokuwa ikiendelea kufanyika katika maeneo yao huku akisisitiza kuwataka kushikamana na mkuu wao wa wilaya popote pale atakapokuwa akiyekeleza shughuli zinazohusu maendeleo.
"Mimi niseme madiwani tunatakiwa kushiriki kwa vitendo misalagambo na wananchi wetu,ukifika eneo la tukio shika jembe na wewe...hii itahamasisha wananchi kutekeleza shughuli zinazoendelea" alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha mwenyekiti huyo aliendelea kusema kwamba halmashauri yake itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wanampatia ushirikiano mkuu wao wa wilaya huku akimpobgeza Rais kwa kumteua kiongozi huyo na kumleta wilayani Korogwe.
Vilevile mwenyekiti huyo wa halmashauri amemtaka mkaguzi wa ndani kujidhatiti sanjari na kuongeza mshikamano kwenye utendaji kuiwezesha halmashauri kupata hati safi badala ya ile yenye mashaka.
Kuhusu fedha za wanawake na vijana mwenyekiti huyo wa halmashauri alisema kwamba kiasi cha shilingi mil 15 zimetengwa kwa ajili ya kutolewa kwa makundi hayo maalum katika jamii.
Mbali na hilo mwenyekiti huyo aliishauri serikali kuangalia uwezekano wa utekelezaji wa fedha za miradi kwa wakati hatua ambayo itawezesha kufanikisha shughuli zilizopangwa kufanyika na kuharakisha maendeleo.
Alisema,kuchelewa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hatua ambayo inalenga kuwaongeza ari wananchi katika kuendelea kushiriki utekelezaji wa miradi ya jamii.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa