1. KITUO CHA AFYA MKUMBARA
Ujenzi wa kituo cha Afya Mkumbara. Ujenzi huo upo katika hatua ya msingi. Jumla ya sh. ml. 500 zitatumika katika ujenzi huo. Uwepo wa kituo hicho cha afya utasaidia kutatua kero za wananchi katika huduma za Afya. Fedha hizi ni kwa ajili ya ujenzi wa majengo kumi na mbili (12) yakiwemo Utawala, kliniki ya mama, baba na mtoto, kichomea taka, wodi ya wazazi, wodi ya watoto, wodi ya wanawake, wodi ya wanaume, maabara, OPD, Theater, chumba cha kuhifadhi maiti na CTC.
2. Mradi wa Maji Kijiji cha Mkokola
Mradi huu unafadhiliwa na World Vision Tanzania ambapo shughuli zilizopangwa kutekelezwa nikusanifu mradi na kusimamia kazi ambazo zinafanywa na wataalam wa Halmashauri na kazi nyingine zinafanywa na Mkandarasi ambaye ana mkataba na World Vision Tanzania ambazo ni:
1. Kujenga kibanda cha pampu, kuchimba kisima
2. Kulaza mtandao wa bomba kubwa kutoka kwenye kisima hadi kwenye tanki
3. Kujenga tanki la kuhifadhia maji lita 50,000
4. Kusambaza mtandao wa mabomba kwenye vituo
5. Kujenga vituo 12 na kufunga pampu, kuchimba kisima cha mita 110 ambacho kina uwezo wa kuhudumia watu 3000.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa