Na Omary Mwinjuma,Korogwe DC
Maelekezo hayo yamesemwa na menejimenti ya Mkoa wa Tanga Wakati wa kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Korogwe.Menejimenti hiyo ikiungana na timu ya wataalamu wa halmashauri ya wilaya ya Korogwe walitembelea miradi mbalimbali ikiwemo ukamilishwaji wa jengo la utawala katika hospitali ya wilaya Makuyuni na ujenzi wa shule mpya ya Msingi katika kata ya Mkomazi ambapo shughuli za ujenzi bado zinaendelea.
Aidha Menejimenti hiyo ilitembelea kikundi cha wanufaika wa mkopo 10% cha Tunajali kilichopo kata ya Makuyuni kinachojishughulisha na shughuli za upishi na Ukodishaji wa Maturubai.Hapa Menejimenti ilikipongeza kikundi hicho kwa kufanya kazi kwa ushirikiano mzuri na kufanikiwa kurudisha mkopo huo kwa wakati.Vilevile imevitaka vikundi vingine kujifunza kutoka katika kikundi hicho ili kuweza kuwa na mafanikio mazuri na kuhimiza mshikamano Zaidi yao.
Kwa upande wa kikundi wameshukuru serikali ya awamu ya sita kupitia uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe,huku wakiomba wapatiwe tena mkopo mara baada ya kumaliza kurejesha ili waweze kununua usafiri wao ambao umekuwa ni kikwazo katika huduma wanayoitoa kwa jamii.


Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa