Hayo yamesemwa leo na Mbunge wa jimbo la Korogwe vijiji Mhe. Timotheo Paul Mzava ikiwa ni katika vikao vyake na makundi mbalimbali mara baada ya kuchaguliwa katika awamu nyingine.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya kikiuzuriwa na viongozi wa kisiasa,kamati ya ulinzi na usalama na viongozi wa serikali.
Mhe. Mnzava amewataka wenyeviti hao kushirikiana na wataalamu ipasavyo ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wananchi kisha akakemea tabia ya baadhi ya Wenyeviti hao kuuza ardhi kiholela kupitia nafasi zao.
Kwa upande mwingine Kaimu Mkurugenzi Bi. Helen Mshana aliwakumbusha wenyeviti hao kufanya vikao vya kisheria kwa utaratibu akisisitiza suala zima la kusoma mapato na matumizi kwa Wananchi.
Nae Katibu wa Chama cha Mapiduzi Jimbo la Korogwe Vijijini Bi.Safina Nchimbi amewaambia viongozi hao kwenda kutoa ushirikiano wa kutosha Wananchi akisisitiza suala la kulinda Amani kwani uchaguzi umeshapita sasa ni wakati wa kuijenga Nchi kimaendeleo.

Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa