Maneno hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Mhe. Selemani Mwongozo wakati kuunda baraza jipya la madiwani litakalotumikia kwa miaka mitano baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wakati Mhe. Emmanuel Mng’ong’ose akiteuliwa kuwa Makamu wake.Waheshimiwa Madiwani hao wameapa leo mapema tayari kwenda kuunaza majumu yao mapya.Katika kundio hilo linalojumuisha madiwani wapya na wa Zamani.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mhe. Timotheo Mnzava, ametoa matumaini mapya kwa wananchi wa Wilaya ya Jimbo la Korogwe Vijijini akiahidi ushirikiano thabiti kwa uongozi wa baraza jipya la Madiwani, Katika hutua yake hiyo alisisitiza kusimamia ipasavyo maendeleo ya Wananchi wa korogwe Vijijini.
Sanjari na hayo Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe.William Mwakilema amewapongeza Madiwani hao kwa kuchaguliwa tena kuwatumikia wananchi.Aidha Mheshimiwa Mwakilema akatoa Wito kwa Madiwani Kuongea na Wananchi kutunza amani ya Nchi hasa katika kipindi hichi ambacho nchi ilipitia kwenye changamoto.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe alipokea pongezi za waheshimiwa madiwani kwa kusimamia mapato katika kipindi ambacho hawakuwepo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano mzuri ili kuendelea kuongeza mapato ya halmashauri yetu.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa