UTANGULIZI:
Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ni kati ya Halmashauri tisa katika Mkoa wa Tanga. Kiutawala ina Tarafa nne za Mombo, Bungu, Magoma na sehemu ya Tarafa ya Korogwe, Kata 29 na vijiji 118 pamoja na Vitongoji 610. Kati ya Kata hizo Kata ya Mombo ni Mamlaka ya Mji Mdogo kuanzia mwaka 2005 na ina Vitongoji 20.
Halmashauri ina eneo la kilomita za mraba 3,544 ambapo kilomita za mraba 1,334 au asilimia 37.6 ya eneo lote linafaa kwa kilimo. Eneo la Halmashauri ni asilimia 12.9 ya eneo la Mkoa wa Tanga ambalo ni kilomita za mraba 27,348. Idadi ya wakazi kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 ni watu
242,038 wakiwemo wanaume 118,544 na wanawake 123,494. Kwa mwaka 2016 idadi ya watu inakadiriwa kuwa 264,050 yaani wanaume 129,325 na wanawake 134,725 sawa na wastani wa watu 4.5 kwa Kaya. Ongezeko la idadi ya watu kwa mwaka kutokana na Sensa ni asilimia 2.2 kwa mwaka.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa