Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mhe. Timotheo Paul Mnzava akutana na Walimu wakuu wa shule za Msingi na Sekondari pamoja na Maafisa elimu kata ikiwa ni katika muendelezo wa Vikao vyake na Makundi mbalimbali kusikiliza changamoto zinazikabili makundio hayo.
Katika kikao hicho Mhe. Mnzava aliwapongeza Walimu hao kwa kufanya kazi kwa kujituma saana na hasa katika kusimamia miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa katika shule zao.Mbali na sifa hizo Mhe. Mnzava hakuacha kuwakemea baadhi ya Walimu kwa kufanya mambo kinyume na maadili ya ualimu yanavyotaka akigusia suala la walimu kuwa walevi,watoro kazini na tabia ya kutembea na Wanafunzi.
Kwa upande wa Walimu nao walitoa changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo masuala ya Maslahi yao pamoja Motisha ili kuchagiza kufanya kazi kwa bidii,Ufinyu wa fedha kwa ajili ya kuendesha shule,Upungufu wa Madawati pamoja na Miundombinu chakavu ya Madarasa.Aidha Walimu hao walimuomba Mbunge huyo kuwaasa Wananchi Pindi wanapokuwa Majukwaani juu ya umuhimu wa elimu na kuwa na ushirikiano Mzuri na Walimu hao.

Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa