Maafisa elimu kata mjiandaye....
Ni kuhusu mgao wa pikipiki ambazo tayari zimepokelewa na halmashauri yenu ya wilaya ya Korogwe.
Pichani anaonekana Dk George Nyaronga ambaye ni mkurugenzi mtendaji wenu,amesema pikipiki hizo zimetolewa na Tamisemi ili kiwarahisishia utendaji kazi.
Dk Nyaronga amesema,anaamini kwamba ujio wa zana hizo za kazi itasaidia kuhakikisha kiwango cha elimu kinapanda.
Kwa mujibu wa Dk Nyaronga anaamini kwamba pikipiki hizo zitatumiwa na maafisa elimu kata katika kuleta matokeo chanya kwa elimu ya msingi na sekondari.
Amesema,pikipiki hizo zinapaswa kutumika kwa shughuli za kikazi tu na si vinginevyo akiwataka wahusika kuzitunza ili zidumu kwa muda mrefu na kuleta tija kwa jamii.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa