Hayo yamesemwa leo wakati wa ukaguzi wa Miradi uliofanywa na kamati ya fedha ya Halmashauri ya wilaya ya Korogwe.Takribani Miradi Saba imekaguliwa leo na kamati ya fedha ikiwemo Miradi Mitatu Katika tarafa ya Mombo ikiwa ni Ukarabati wa Nyumba moja ya mwalimu na Vyumba sita (6) vya madarasa katika Shule ya Msingi Mkalamo,Ujenzi wa vyumba vitatu (3) vya madarasa na matundu sita (6) ya vyoo katika shule ya Msingi Makuyuni na ujenzi jengo la utawala la halmashauri ya wilaya ya korogwe.
Aidha katika tarafa ya Magoma kamati ilikagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari Makorola,kadhalika ujenzi wa matundu kumi na sita (16) ya vyoo shule ya msingi Sekioga,Nyumba ya mwalimu,madarasa manne (4),mabweni manne (4) na matundu ya vyoo kumi (10) katika shule ya sekondari Foroforo pamoja na ujenzi wa chumba kimoja (1) na matundu nane (8) ya vyoo katika shule ya sekondari Mashewa.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa