UTARATIBU WA KUTOA LESENI
Leseniya Biashara
Hiki ni kibali maalum cha Serikali kinachotolewa kwamfanyabiashara yeyote anapotaka kufanya biashara hapa nchini. Sheria ya Leseniza Biashara Na. 25 ya 1972 – Kifungu cha 3(a) kimeweka bayana kuwa, Kibalihicho maalumu kinaitwa Leseni ya Biashara. Kwa hiyo basi, kufanya biasharayoyote bila kuwa na kibali hiki ni kosa la jinai.
IliMwombaji Apate Leseni Ya Biashara Anapaswa Kumbatanisha Nyaraka Zifuatazo:
· Nakala ya hati ya kuandikisha jina laBiashara au Kampuni (Photocopy of Certificate of Incorporation or Registration& Extract);
· “Memorandum, and Articles ofAssociation” ambazo zitaonyesha kuwa Kampuni imeruhusiwa kisheria kufanyabiashara inayoombwa, pamoja na majina ya wamiliki wa kampuni, hisa zao nautaifa wao;
· Uthibitisho wa uraia kwa kuwasilisha,nakala ya hati ya kusafiri nje ya nchi ya Tanzania au hati ya kusafiri katikanchi za Afrika Mashariki, cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo (Affidavit)kuonyesha kuwa ni Mtanzania, na kama mgeni alete hati ya kuishi nchini darajala kwanza (Residence Permit Class A).
· Endapo wenye hisa wote wapo nje yanchi itabidi maombi yaambatane na hati ya kiwakili (Power of Attorney) ya kumpamamlaka raia wa Tanzania, raia wa kigeni mwenye hati ya kuishi nchini daraja“A” au hati ya kufanya kazi nchini daraja “B” zinazoainisha kuwa anasimamiakampuni husika.
· Nakala ya ushahidi wa maandishi kuwaana mahali pa kufanyia biashara (lease agreement, Title deed, Certificate ofoccupancy, e.t.c);
· Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi(Tax Payer Identification Number - TIN).
UtaratibuWa Kupewa Leseni:
Jaza fomu ya maombi ya Leseni (TFN 211 ya 2004)
· Ambatanisha nyaraka kama ilivyoainishwa hapo juu kwa ajiliya ukaguzi (assessment) na kujulishwa kiasi cha ada cha kulipa
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa