Kilimo Kama mhimili mkuu wa uchumi wa Halmashauri, ni chanzo cha kipato na uchumi wa kaya kwa zaidi ya 80% ya wakazi wake.
Halmashauri inazo hekta 116,339 (sawa na 32.8% ya eneo lote la Halmashauri) zinazofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali.
Kwa ujumla wakazi wa maeneo ya vijijini hujishughulisha na kilimo cha mazao ya biashara na chakula katika maeneo madogomadogo. Kwa wastani mkulima/kaya moja humiliki kati ya hekta 0.5 hadi 2 za mazao ya chakula na biashara.
Mazao muhimu ya chakula yanayolimwa katika Halmashauri ni pamoja na mpunga, mahindi, muhogo, viazi vitamu, viazi vikuu, maharage na ndizi. Mazao ya biashara yanayolimwa ni mkonge, chai, mboga, matunda ya tropiki, na korosho. Aidha kwa kiasi kidogo mazao kama kahawa, iliki na pamba pia hulimwa
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa