Sunday 31st, August 2025
@Morogoro
Nane Nane ni sikukuu ya wakulima nchini Tanzania ambayo huwapa fursa wakulima, taasisi na wadau mbalimbali wa kilimo kote nchini kuonesha bidhaa zao na mafanikio yao katika mwaka husika.
Sikukuu ya maonyesho ya wakulima iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1977 ili kuongezea nguvu sera ya Serikali ya wakati huo ya ‘ Siasa ni Kilimo ‘, ambapo wakulima katika wilaya, mkoa na kitaifa walionesha mazao yao halisi ya kilimo, wakaonyesha pembejeo za kisasa za killimo pamoja na kufundishwa namna ya kutumia pembejeo hizo kwa ustawi wa kilimo na taifa.
Sikukuu ya Wakulima NaneNane kwa Kanda ya Mashariki ikuhusisha Mikoa ya Dar es salam,Pwani,Tanga na Morogoro inaadhimishwa kila mwaka Katika Viwanja Vya NaneNane Morogoro.
Kaulimbiu ya Mwaka huu : Chagua Kiongozi bora kwa Maendeleo ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi 2025
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa