Mwakilishi huyo ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe amewataka wanaoendesha Mashirika yasiyo ya Kiserikali kufuata Sheria za Nchi husika na miongozo inayotolewa na Serikali wakati wanapotekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo .
Bw. Ngulungu alitoa kauli hiyo kwenye Ufunguzi wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Serikali (NGO`s). Ufunguzi huo umefanyika Julai 01, 2025 Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Siku ya Jumanne ukiwakutanisha wadau mbali mbalimbali kutoka halmashauri ya Wilaya na Halmashauri ya Mji Korogwe.
Wakati huo Msajili Msaidizi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO`s) Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Bw. Joseph Gweba alisema kuwa lengo la kikao hicho cha Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali ni kuwapitisha Wajumbe katika kuwasilisha na Kujadili mchango wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO`s).
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa