Mafunzo haya yameanza leo katika shule ya Msingi Gereza kupitia program ya shule bora kumuunga mkono Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan yakiwa na lengo Kuhifadhi mazingira na utumiaji wa nishati safi
Akifungua Mafunzo hayo Muwakilishi wa Afisa Elimu Msingi Mwl. Marietha Hipolite amesema Mradi huu utarajiwa kutekelezwa kwenye kata 10 za Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ukihusisha uanzishwaji wa Vitalu vya Miti pamoja matumizi ya Nishati safi ya kupikia. akiwapitisha kwenye Mafunzo hayo Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Bwn. Titus Muyombo Amesema kuna umuhimu mkubwa sana wa kutunza Kutunza mazingira safi na salama shuleni
Mafunzo haya ya siku mbili yanatarajiwa kuwajengea uwezo Walimu wa kuu na walimu wa Mazingira Kusimamia vyema suala la utunzaji wa Mazingira shuleni pamoja na maeneo jerani yanayozunguka ili yaweze kuwa salama kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa