Tuitunze misitu kwa faida ya kizazi cha sasa na baadae pamoja na kuongeza uchumi wa mtu mmoja moja na taifa kwa ujumla,hayo yamesmwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Wakili.Goodluck Mwangomango wakati wa ufunguzi wa sherehe za kuadhimisha miaka 40 ya Shirika la Kidini DANMISSION ambalo linafanya kazi pamoja na shirika la Tanzania Forest Conservation Group (TFCG) katika upandaji na uhifadhi wa misitu .
Wilaya ya Korogwe imepata bahati ya kuwa sehemu ya Mradi wa uhifadhi wa mazingira kupitia shirika la Tanzania Forest Conservation Group (TFCG),ambapo miradi hii inatekelezwa katika kata ya Lewa-Kijiji cha Mashindei na Kata ya Vugiri.Wakazi wa vijiji hivyo wamenufaika na mradi huo ambapo wamepewa elimu ya utunzaji wa Misitu pamoja na kuanzisha kilimo cha Viungo mbalimbali ambapo Wananchi wameanza kufanya kilimo hicho.
Mkurugenzi wa Tanzania Forest Conservation Group (TFCG) Ndugu.Charles Meshack amemshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kwa Ushirikiano walioupata katika kutekeleza Mradi huo na kuendelea kuwasihi Wananchi wa korogwe kuendelea kuitunza miradi hiyo.
Kwa upande wa Wananchi wa Wilaya Korogwe wamesema wamefurahishwa sana na mradi huo kwani umewaongezea kipato pamoja na kupata ujuzi mzuri katika kuhifadhi mazingira ya misitu na kutumia nishati safi ikiwa ni kumuunga Mkono DKT. Samia Suluhu Hassan katika kampeni ya kuhifadhi mazingira na matumizi bora ya nishati safi.
Na Omary Mwinjuma KorogweDC
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa