Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Mheshimiwa Yusuph Kallaghe leo ameongoza wajumbe wa baraza la Madiwani ambapo leo hii kulifanyika Baraza la Taarifa za Kawaida na Baraza la Tathimini kwa pamoja.
Mabaraza hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Zamani wa Halmshauri uliopo Korogwe Mjini,aidha katika Baraza la Taarifa Wajumbe walijadili na kupitisha Taarifa mbalimbali zikiwemo za miradi na nyinginezo.Sambamba na hayo waheshimiwa madiwani walipiga kura Kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ambapo Mheshimiwa Muhidini Rajab alichaguliwa tena kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
Aidha Katika Baraza la Tathmini Mheshimiwa Yusufu Kallage Alisisitiza Kukamilika kwa miradi kabla ya kuanza kwa robo nyingine ya mwaka.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa