Na Omary Mwinjuma
Cheti hicho kimetolewa leo na Meneja wa Benki ya NMB tawi la Mombo Bi.Asha Mlawa katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Wakili.Goodluck Mwangomango iliyopo Makuyuni ambapo wakuu wa idara na vitengo mbalimbali walihudhuria makabidhiano ya cheti hicho.
Bi.Mlawa amesema Benki hiyo inatambua mchango wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe na kuiunga mkono hasa katika maendeleo ya miradi mbalimbali ikiwepo katika sekta ya elimu pamoja na afya.
Kwa upande wa Halmashauri Wakili. Mwangomango ameishukuru benki hiyo kwa utambuzi wa kuwa kati ya washirika bora kifedha na kuahidi kuendelea kutoa ushirikia wa kutosha kwa benki hiyo.



Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa