MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Kassongwa ameelezea kuridhishwa kwake na utendaji kazi wa benki ya NMB Tawi la Korogwe akisema imejipambanua ikionyesha dhahiri kwamba imejipanga kuwahudumia wananchi hususani wale wanyonge waliopo maeneo ya vijijini akiwataka kuendelea kupanua wigo.
Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo jana alipohudhuria hafla fupi iliyokuwa na lengo la kufahamiana kati ya uongozi na wafanyakazi wa benki hiyo na viongozi wa serikali wakiwemo wale wa halmashauri mbili za wilaya na mji Korogwe fursa ambayo pia ilitumika kufahamu huduma mpya za kibenki.
Katika mazungumzo yake,mkuu huyo wa wilaya alisema,amefurahi kufika kwenye benki hiyo ikiwa sehemu ya taasisi za serikali ya kwanza kumualika tangu kufika kwake Korogwe na kwamba hata pale alipofuatilia habari zao alizikuta ofisini kwake zikionyesha mahusiano mema kati yao na serikali.
“Nawapongeza kwa kuandaa hafla ya kuwakaribisha viongozi wa serikali,ni hafla ya kwanza kwa taasisi kualika ofisi ya DC ambapo nimekuja na timu yangu na viongozi wetu wa halmashauri wakiwemo wenyeviti,ninazo taarifa juu ya mahusiano yenu kuwa mazuri na serikali,hongereni sana”alisema DC.
Aidha mkuu huyo wa wilaya ya Korogwe alisema kwamba benki hiyo imeonyesha kuwa iko bega kwa began a serikali katika kuhakikisha inafikisha huduma zenye ubora karibu na wananchi ambapo aliwasisitiza kuendeleza kupanua wigo kwa kuhakikisha kwamba wanafikisha huduma kwenye vijiji.
Mkuu huyo wa wilaya aliongeza kusema kwamba,Serikali itaendelea kushirikiana na benki hiyo ya NMB lengo likiwa kuhakikisha kuwa wananchi walio wengi wanapata huduma zenye ubora huku akitanabaisha kwamba milango ya ofisi yake iko wazi pindi watakapokuwa wakihitaji kusaidiwa.
“Niwapongeze kwa kazi nzuri mnazozifanya,mmekuwa bega kwa began a serikali ila niwaombe mjitahidi kufika na kule vijijini ili huduma kuwanufaisha wananchi walio wengi”alisema mkuu huyo wa wilaya ya Korogwe huku akielezea kufurahishwa kwake na taasisi hiyo kuonyesha mshikamani na serikali.
Meneja wa benki hiyo ya NMB tawi la Korogwe Lugano Mwampeta alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa tayari wamefanikiwa kufika maeneo ya vijijini kwa kuwatumia mawakala ambao wamekuwa wakitekeleza majukumu ya msingi ya kibenki huku wakipata kamisheni nzuri na yenye kuridhisha.
Mbali na hilo Mwampeta aliueleza ugeni huo uliotembelea ofisi hizo za NMB kuwa hivi sasa kuna huduma mpya inayojulikana kama NMB Kliki ambayo mteja kutumia simu yake ya kiganjani kwa ajili ya kupata huduma za msingi njia ambayo pia aliieleza kuwa inakuwa rahisi kwa mtu kufungua akaunti.
Katika hafla hiyo fupi iliyokwenda sambamba na kifungua kinywa,wageni waliohudhuria ni mkuu wa wilaya ya Korogwe na kamati yake ya ulinzi na usalama,wakurugenzi wa halmashauri za mji na vijijini,meneja uhusiano idara za serikali benki ya NMB kanda ya kaskazini na wafanyakazi wa benki hiyo.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa