Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kwa kupata Hati safi kutoka kwa Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Miaka mitano (5) mfululizo pamoja na ukusanyaji mzuri wa Mapato kwa kuvuka lengo la ukusanyaji Mh Balozi Dkt. Batilda Burian ametoa pongezi hizo katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kupitia Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),kilichofanyika leo tarehe 14 Juni 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Korogwe.Katika Kikao hicho Dkt. Batilda Burian aliagiza Menejimenti chini ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kuhakikisha hoja zote za Ukaguzi zilizowasilishwa zinajibiwa kwa vielelezo kikamilifu hadi ifikapo Juni 30, 2025.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe.William Mwakilema Katibu Tawala Wilaya ya Korogwe Bi. Mwanaidi Rajabu, Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa pamoja na ya Wilaya, Maafisa kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,Waheshimiwa Madiwani Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya Korogwe,Wakuu wa Idara na Vitengo.
Sanjari na hayo Mkuu wa Mkoa wa Tanga amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Wakili.Goodluck Mwangomango na Menejimenti yake kwa kufanya kazi kwa Ushirikiano Mzuri wenye kuleta mafanikio huku akitoa maelekezo kwa Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa jamii pamoja na Sheria kuwatembelea Wananchi ili Kuwa kiunganishi kati ya Wananchi na Serikali.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa