Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe.William Mwakilema ameipongeza Halmashauri kwa kusimamia lishe huku akihimiza jamii kuzingatia lishe bora ili kuweza kuwa na afya njema kuepukana na maradhi ya utapia mlo pamoja na afya dhohofu.Mhe.Mwakilema ameyasema hayo wakati wa kikao cha tathmini ya lishe cha robo ya kwanza ambacho kimefanyika leo katika ukumbi wa Halmashari ya wilaya ya Korogwe Uliopo Mkuyuni kikihusisha wataalamu mbalimbali na watendaji wa kata.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Adv. Goodluck Mwangomango amewashauri wataalamu wa lishe kuweka Ratiba ili kuweza kutoa elimu kuanzia shuleni na ngazi ya kata juu ya suala la lishe Bora kwa jamii.
Katika kikao hicho baadhi ya wajumbe walitoa maoni wakipendekeza kuanzisha klabu za lishe shuleni ili wanafunzi waweze kujifunza mambo mbalimbali yatokanayo na lishe Pamoja kuwa na matamasha mbalimbali ili kuijenga uwezo yakinifu wa masuala ya lishe.

Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa