Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijiji Mhe.Timotheo Mnzava akabidhi mfano wa Hundi kwa vikundi vya Wajasiliamali ambapo Jumla ya Vikundi 11 Vimepatiwa mkopo huo wa asilimia 10 wa Halmashauri utakaowasaidia Wananchi wa korogwe kujikwamua Kiuchumi kwa kufanya biashashara mbalimbali
Katika halfa Hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ulipo Makuyuni ikihudhuriwa na wataalama wa halmashauri ya wilaya ya Korogwe.Mhe.Tumotheo Mnzava amewaasa wana vikundi hao kwenda kuzitumia fedha walizokabidhiwa kwa malengo waliombea kupata mkopo na kuzirudisha kwa wakati fedha hizo ili ziweze kuwasaidia na wanavikundi wengine.
Sambamba na hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya korogwe wakili.Goodluck Mwangomango amewataka kulipa kodi pindi watakapofungua biashara zao ili kuweza kuchangia pato la Halmashauri.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa