Na Omary Mwinjuma
Waratibu elimu na Walimu waandelea kunolewa kuongeza mbinu bora za ujifunzaji na ufundishaji ili kuongeza za ufaulu wa wanafunzi wa shule za msingi kupitia programu ya Shule bora kushirikiana na Serikali ya Tanzania. Mafunzo hayo yameanza leo katika shule ya msingi Boma iliyopo Korogwe Mji yakiwa na lengo la kuongeza ufaulu na kupunguza mdondoko wa wanafunzi shuleni.
Akiongea na Wataalamu hao Afisa wa Mradi wa Shule Bora Mkoa wa Tanga Bwn. Marsel Salema amewaambia walimu hao wakawe wabunifu hasa katika kutengeneza mazingira bora ya kufundishia na Kujifunzia ili kuweka mahusiano mazuri kati ya Mwalimu na Mwanafunzi ili kujenga hari ya kujifunza Zaidi.
Aidha kwa upande wa wanufaika wa programu hiyo wamesema wanaishukuru sana serikali kupitia mradi huo wa shule bora kwa kujengewa uwezo mzuri na mbinu bora za kujifunzia na kufundishia ili kwenda kuleta tija kuinua sekta ya elimu Nchini,sambamba na hayo walimu hao wameahidi kwenda kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu ikiwemo kusambaza maarifa hayo kwa walimu wengine waliopo shuleni.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa