Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe.William Mwakilema wakati wa uzinduzi wa Mikopo ya Asilimia kumi(10%) Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe.Katika uzinduzi huo aliambatana na Katibu tawala wa Wilaya ya Korogwe Bi. Mwanaidi Rajab na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Ndugu. David Mpumilwa.
Katibu tawala alizungumza na Vikundi akiwasii kuwa waaminifu na kuchapa kazi ili kujikwamua kiuchumi .
Katika Uzinduzi huo Vikundi 13 vikihusisha Kundi la Walemavu,Vijana na Kundi la Wanawake ndio vimekizi vigezo vya kupata Mkopo huo kwa awamu ya kwanza.Kiasi cha Fedha Shilingi Milioni 250 zinatarajiwa kukopeshwa kwa vikundi mbalimbali ambavyo vitakuwa vimekidhi vigezo vya kupata Mkopo huo.
Aidha Wawakilishi kutoka katika Makundi yote Matatu Walishukuru Serikali ya awamu ya Sita kupatiwa Mikopo hiyo ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi huku wakizidi kuomba kupatiwa elimu zaidi ya Ujasiliamali ili kuweza Kusimamia vizuri Miradi ambayo wanaenda kuitekeleza.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa