Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Mhe.Yusuph kallaghe wakati wa Ufunguzi wa kikao cha uwekaji saini katika mikataba ya uhifadhi wa misitu unaofanywa na taasisi ya kuhifadhi misitu ya asili Tanzania (TFCG).Katika halmashauri ya wilaya ya Korogwe mradi huu unatekelezwa katika kata ya Vugiri kwenye vijiji vitatu na Kata ya Lewa kwenye kijiji kimoja.
Mradi huu unatarajiwa kuwa na mafanikio chanya kwenye mazingira hasa kuwanufaisha wananchi kwenye maeneo yanayozunguka mradi huu.
Sambamba na hayo mheshimiwa kallaghe amempongeza Dkt.Samia Suluhu Hassan katika mpango wa kuondoa matumizi ya kuni na mkaa hadi ifikapo mwaka 2030.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa