Hayo yamesemwa na mmoja wa timu ya waratibu wa kifua Kikuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Daktari. Baraka Mbwambo wakati akitoa elimu ya Ugonjwa kifua kikuu kwa wananchi wa Kata ya Mkalamo kijiji cha Kwaisewa. Alisema Ugonjwa wa kifua kikuu ni ugonjwa wa Kuambukizwa kwa njia ya hewa kwa kuvuta yenye bakteria ambapo unashambulia sehemu za mapafu.
Daktari Baraka alisema watu wanapaswa kubadilika na kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara dhidi ya magonjwa yanayoambukiza ili kuepuka athari zaidi mara baada ya kupata maambukizi kwani magonjwa kama hayo yanatibika kwenye vituo vyetu vya afya pindi unapowahi matibabu.
Sambamba na elimu iliyotolewa, Wanachi walijitokeza kupima Afya zao ili kubaini ambao wana dalili ya ugonjwa wa kifua kikuu.Kampeni hii inaendelea kufanyika kwenye maeneo mengine Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ili kubaini wagonjwa na kuwapatia matibabu mara baada ya kugunduliwa kuwa na maambukizi.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa