Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji leo tarehe 09 Januari 2025 amekagua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali inayotekelezwa katika halmashauri wilaya ya korogwe ambapo amesema fedha za miradi ya maendeleo zilizopelekwa katika halmashauri ya Wilaya ya Korogwe zimesimamiwa kikamilifu kutekeleza miradi hiyo.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika Kata ya Magoma - Kijiji cha Makangara, mara baada ya kufanya ukaguzi wa miradi hiyo.Amesema hayo baada ya baadhi ya wananchi wa Magoma kukiri kuridhishwa na maendeleo ya miradi inayotekelezwa katika tarafa hiyo.
Katika ziara hiyo Mhe. Dkt. Kijaji ametembelea, amekagua na kuweka mawe ya msingi ya miradi ya ujenzi ya madarasa na matundu ya vyoo katika shule mpya ya sekondari Makorola na ujenzi wa mabweni shule ya sekondari Foroforo pamoja na ujenzi wa nyumba ya Afisa Ugani Kata ya Magoma.
Aidha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amewashukuru Wanakorogwe kwa mapokezi mazuri wakati wa ziara hiyo katika Wilaya ya Korogwe akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutembelea miradi inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita katika Mkoa wa Tanga, huku akitaja kaulimbiu ya “Waone na Wasikie.”
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa