Mafunzo hayo yametolewa yakiwahusisha wakufunzi kutoka katika vyuo vya ualimu Mpwapwa(Dodoma) na Korogwe(Tanga).Mafunzo yameendeshwa kupitia Program ya shule bora inayofadhiliwa na nchi ya Uingereza kupitia UKAid yamehitimishwa leo tarehe 31 januari 2025.
Mafunzo yalifanyika kwa muda wa siku nne katika shule ya msingi Gereza iliyoko kata ya magila gereza.TEZRA MKAMA (Muwakilishi Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia) aliwasisitiza Walimu kuyatumia vyema mafunzo waliyopatiwa ili kuweza kuinua somo hilo la Hisabati na kuleta manufaa katika kuongeza ufaulu kwa taifa na kuwa wawakilishi bora kwa walimu waliopo shuleni kupata maarifa hayo.
Aidha Walimu waliombwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa maafisa wa Wizara Pindi wanapopita wakati wa ufuatiliaji hasa katika kipindi hichi cha maboresho ya mtaala wa elimu.Sambamba na hayo walimu walitoa shukran kwa serikali ya awamu ya sita kwa kuwezeshwa kupata mafunzo hayo.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa