Wakina Mama zaidi ya Hamsini wapata elimu ya Afya ya mama na Mtoto pamoja na elimu lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe.Elimu hiyo imetolewa kwa kushirikiana na taasisi ya USAID pamoja na wataalam wa Afya wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe.
Maradi huu umeanzishwa utatekelezwa kwa miaka 5 chini ya Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na ufadhili wa shirika la Kimarekani USAID ikiwa na lengo la kuhamasisha tabia chanya kuhusu malezi ya Watoto wachanga kufuatia maelekezo ya wataalam wa afya.Mradi huu unarajia kufanyika hapa Nchini katika Mikoa 11 wakati katika Mkoa wa Tanga mradi huu Utatekelezwa kwenye wilaya zote na Halmashauri 11 kupitia idara ya afya.
Aidha katika mafunzo hayo Wataalamu wa afya wanatarajia kuwepo na mabadiliko katika namna ya malezi ya Watoto hasa walio chini ya umri wa Miezi sita ili kuweza kuimarisha afya za watoto na Kuepusha magonjwa nyemelezi ikiwemo Malaria.
Wakina Mama hao baada ya kupata elimu hiyo walikiri kuzingatia maelekezo hayo yaliyotolewa na wataalamu na kuacha kuishi kimazoea
ili kuboresha afya za Watoto wao.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa