Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Mhe. Sadiki Kallaghe wakati wa kikao cha Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango kilichofanyika leo tarehe 19 Juni 2025 ambapo alitilia mkazo Ukusanyaji wa mapato kikamilifu katika halmashauri kipindi ambacho uongozi wao utakuwa umekoma,Matumizi bora ya Fedha pamoja na usimamizi makini wa Miradi ya Maendeleo.
Sambamba na hayo Mhe. Mwenyekiti aliwahusia Watumishi kupendana na kufanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu ili kuweza kuisimamia Halmashauri katika misingi imara yenye kuchagiza maendeleo kwa jamii.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa