WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi akimambatana na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Mhe.Timotheo Mzava ,Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe.William Mwakilema wamaliza mgogoro baina ya Wamiliki wa Shamba la Sisal Estate na Wananchi wa Kata ya Kwashemshi Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga uliodumu kwa zaidi ya miaka 30.Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa eneo hilo, Mhe. Ndejembi amesema baada ya kufanya vikao na mwekezaji huyo, makubaliano yalifikiwa ya kuwapatia wananchi hao ekari 100 kwa ajili ya Makazi na matumizi mengine ambayo yatapangwa na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa