Halmashauri ya Wilaya Korogwe
Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe imetambua maeneo mahususi kwa ajili ya uwekezaji baaada ya kufanya utafiti wa kina kwenye maeneo kadhaa, Maeneo yaliyotengwa ni Mombo, Mswaha, Mkomazi, na Bwiko.
Hekta 19,286 zinapatikana na zinafaa kwa umwagiliaji na hekta 13,416 zinahitajika kuwekewa miundombinu ya umwagiliaji, Kati ya Hekta 1,000 zilizopo katika bonde la Mafuleta zinazofaa kwa umwagiliaji ni Hekta 500 tu zenye miundombinu na zinatumika kwa uzalishaji na wakulima wadogo.
Mwonekano mzuri na uoto uliopo katika Safu za Milima ya Usambara pamoja na mabonde yenye kuvutia ya Mto Pangani pamoja na upatikanaji wa wanyama mbalimbali vinafanya kuwepo kwa fursa nyingi za kuvutia watalii nakuhitaji uwekezaji zaidi katika sekta hiyo.
Pia fursa ya uwekezaji katika misitu inayopatikana inafaa zaidi kwa ufugaji wa Nyuki. Uwekezeji katika uchimabaji wa madini aina ya gemstone na madini ya viwandani vitakavyo saidia kuchochea maendeleo ya wanakorogwe na taifa kwa ujumla.
Uwepo wa hali nzuri ya hewa na nguvu kazi yakutosha inaifanya kuwa sehemu nyeti yauwekezaji katika Kilimo, Ufugaji, Uchimbaji Madini, Utalii na Biashara.
Baadhi ya maeneo hayajawahi kufanyiwa kazi hasa katika kilimo, uchimbaji na utalii sehemu ambazo zitakuwa ni ardhi yenye uzalishaji chanya kwa wawekezaji watakao wekeza katika maeneo hayo.
Hapana wasiwasi katika swala la soko kwa mazao yatakayopatikana, kwani soko linapatikana ndani ya wilaya, mikoa jirani ya Kilimanjaro, Arusha, Pwani na Dar es Salaam.
alkadhalika mazao kama mpunga yanaweza kuuzwa nchi za jirani kama Kenya na Uganda, Mchele unaweza kuuzwa kwa wingi kwenye taasisi kama Mashule, Vyuo, Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa.
Walengwa katika uwekezaji ni wanajamii wote wa ndani na nje ya korogwe, wafanyabiashara na taasisi, Kwa upande wa uwekezaji katika kilimo, wanahitajika wakulima wa mashamba makubwa ya mpunga na ujenzi wa miundombinu kwa maeneo ambayo hayajaendelezwa na yanafaa kwa kilimo (umwagiliaji).
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa