Waziri ORTAMISEMI Mh. Selemani Jaffo amewaasa wanasiasa kuacha kuvutani wapi itajengwa hospitali ya Wilaya. Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kutembelea eneo mojawapo la Makayuni kati ya matatu yaliyokuwa yametengwa. Mara baada ya kujionea eneo la Makuyuni Mh. Jaffo ameelekeza hospitali hiyo ijengwe katika eneo hilo na sababu kubwa aliyoitoa, eneo hilo lipo katika barabara kuu ya MOSHI - DAR ES SALAAM hivyo ni rahisi kuhudumia wananchi mbalimbali pindi tatizo linapotokea. Pia ni rahisi kwa watu wa Simanjiro na hata wa Same kupata matibabu katika hospitali hii hivyo basi ameelekeza hospitali hiyo ijengwe katika eneo hilo na maandalizi ya awali yanatakiwa yaanze mara moja. Pia ametaka kituo cha Afya Cha Magoma Kuboreshwa zaidi ili kiweze kutoa huduma zote kama za upasuaji kurahisisha huduma kwa watu wa tarafa za Magoma na hata wa Bungu.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa